Rais mstaafu wa Zimbabwe amefariki dunia nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu, amefariki akiwa na miaka 95.
Rais MUGABE ailikuwa rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1987 mpaka 2017 alipotolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.
Raia mmoja wa tanzania anakabiliwa na mashataka baada ya kusambaza maoni yake ya mtandao wa WhatsApp akimuita rais john Pombe magufuli mpumbavu.Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni.
Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetupilia mbali ombi la mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mahakama kuu kanda ya Mwanza kukubali kufunguliwa na kuanza kusikiliza kesi ya kupinga uamuzi wa jeshi la polisi nchini kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. ...
Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa lkatika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.
Alie kuwa mtu humiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu kutoka DRC Congo Jean-Pierre Bemba amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa makosa ya uhalifu wa kivita na dhuluma za ubakaji ...
Mwanamume mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.
Rais mstaafu wa Zimbabwe amefariki dunia nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu, amefariki akiwa na miaka 95.
Rais MUGABE ailikuwa rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1987 mpaka 2017 alipotolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.
Raisi wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaachia huru wafungwa 61 walio hukumiwa kunyongwa ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wafungwa walio hukumiwa kunyongwa kupewa msamaha
Raisi Magufuli ametoa msamaha huo katika sherehe za miaka 56 ya uhuru wa Taifa hilo zilizo fanyika mjini Dodoma ikiwa ni kwa mara ya kwanza zina fanyika nje ya jiji la Dar es salaam
Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba walinda amani 14 wa muungano huo waliuawa na wengine 53 kujeruhiwa baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kati ya waliouawa, angalau wanajeshi 12 walitoka Tanzania.
Katibu mkuu huyo ameshutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita.
Ameitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa.
Wanajeshi zaidi wametumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi.
Bw Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.
"Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.
"Taarifa za mwanzo mwanzo eneo la shambulio eneo la Kivu Kaskazini zinaonesha angalau walinda amani 12 kutoka Tanzania walijeruhiwa na wengine 40 kujeruhiwa, wanne vibaya.
"Na tunafahamu pia kwamba wanajeshi watano wa jeshi la DR Congo waliuawa.
"Natuma salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathiriwa na pia kwa serikali na watu wa Tanzania.
Na nawatakia uponaji wa haraka wote waliojeruhiwa."
Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.
Umoja wa Mataifa unasema waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.
"Natuma salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wanajeshi wa kulinda Amani na wanajeshi wa FARDCwaliouawa au kujeruhiwa," amesema mwakilishi mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo ambaye ndiye pia mkuu wa kikosi cha walinda amani ambacho hufahamika sana kama Monusco.
Awali, katibu mkuu msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeangazia masuala ya kulinda amani alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba "idadi kubwa" ya wanajeshi walikuwa wameuawa.
Bw Jean-Pierre Lacroix alisema wanajeshi zaidi wametumwa eneo hilo na majeruhi wanasafirishwa.
Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) chimbuko lao ni Uganda lakini wametuhumiwa kutekeleza mashambulio na visa vya ukatili eneo hilo la DR Congo.
Source: BBC
ROBERT MUGABE AMEJIUZULU KAMA RAIS WA ZIMBABWE.
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu . Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo. harakati za kumuondoa madarakani rais huyo kupitia bunge kumesitishwa.
MOTO SHIRIKA LA HABARI CLOUDS MEDIA TANZANIA:
Jeshi la zima moto limefika katika jengo la kituo cha habari cha Clouds Media Group mjini Dar es salaam kudhibiti moto uliozuka katika mojawapo ya vyumba vya kurushia matangazo ya televisheni.
Chanzo cha moto hadi sasa bado hakijafahamika.Tayari moto umeshadhbitiwa.
Hamna majeruhi wala vifo na thamani ya uharibifu haijafahamika bado.
Kiasi ya watu watano wameuawa baada ya kutokea makabiliano kati ya polisi wa Kenya na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga. Polisi walifyatua risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kuzuia msafara wa Odinga uliokuwa ukitoka uwanja wa ndege. Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamewalaani polisi, kwa kuwa na upendeleo katika mzozo wa kisiasa na kikiuka katiba kwa kuwazuia wafuasi wa upinzani kukusanyika.
AU: HATUTORUHUSU KUONA MAPINDUZI YA KIJESHI ZIMBABWE.
Rais wa Guinea ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) amekariri msimamo wa muungano huo na kusema hautakubali
"mapinduzi ya kijeshi" Zimbabwe, shirika la habari la AFP limemnukuu akisema.
"Tunataka katiba iheshimiwe na mfumo wa utawala wa kikatiba urejeshwe. Hatutakubali mapinduzi ya kijeshi."
Tunafahamu kwmaba kuna matatizo ya ndani. Haya yanafaa kutatuliwa kisiasa ndani ya chama cha Zanu-PF na si kwa uingiliaji wa jeshi"
Source: bbc swahili
Watu watatu wamepigwa risasi na kufa leo mjini Nairobi, polisi walipokuwa wanawatawanya maelfu ya wafuasi wa upinzani waliokuja kummpokea kiongozi wao Raila Odinga aliyerejea nyumbani kutoka ughaibuni. Watu hao watatu, ambao ni wanaume, miili yao imeonekana barabarani huko Muthurwa, kitongoji kilichoko kwenye mji mkuu ambako polisi waliokuwa na hewa za kutoa machozi na mabomba ya maji na bunduki za rashasha walikabliana na waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe. Raila odinga amerejea nyumbani leo baada ya ziara ya siku kumi nchini Marekani na Uingereza ambako alikwenda kutafuta uungaji mkono wa madai yake kutaka uchaguzi wa rais urudiwe upya nchini Kenya.
Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo lingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Watu kadhaa wamefariki dunia leo baada Ndege ya kampuni Coastal Air kuanguka eneo la Creta ya Embakai ndani ya mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro,endelea kufuatilia ukurasa wetu kwa Habari zaidi juu ya tukio hili.
Muungano wa upinzani nchini Kenya umekuwa ukifanya maandamano katika maeneo kadhaa nchini kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi IEBC, kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa oktoba
Kaimu waziri wa usalama Fred Matiang'i amesema hatua hiyo imetokana na ukosefu wa nidhamu wakati wa maandamano hayo hali ambayo amesema imeendelea kuathiri biasahara katika miji hiyo.
David Wafula anaarifu.
Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamempatia katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu siku tatu kujisalimisha kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake, afisa mkuu wa polisi anayesimamia maeneo maalum bwana Lazaro Mambosasa amesema kuwa Sheikh Ponda alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na wanahabari .
The Citizen limenukuu kamanda huyo wa polisi akisema kuwa matamshi yaliotolewa na kiongozi huyo wa dini yaliidharau serikali .
Bwana Mambosasa ameongezea kwamba ni sharti ajisalimishe kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo atajipata katika matatizo.
''Ninamshauri Sheikh Ponda kujisalimisha kwa sababu hata akitoroka haitamsaidia kwa sababu tutamkamata'', alisema Mambosasa.
Aliongezea: Alijua kwamba anavunja sheria, wakati alipotoa matamshi ya uchochezi na sasa ajiandae kukabiliwa kisheria.
Kiongozi huyo wa dini amekuwa akijikuta katika mikono ya sheria mara kwa mara kila anapotoa matamshi yake.
Rais Magufuli afanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, Juliana Shonza aula
MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI
Mawaziri 21zimeongezeka Nafasi 2
Manaibu 21 zimeongezeka 5
Utumishi - Mkuchika
Nishati - Kalemani - Mgalo
Madini - Mfuruki - Nyongo
Ujenzi - Mbarawa - Nditie na Kwandikwa
Fedha - Mpango - Kijaji
Katiba na Sheria- Prof. Kabudi
Habari - mwakyembe - Honza
Ndani - nchemba - Masauni
Maliasili - Kigwangala - Kasunda
Ardhi - Lukuvi - Mabula
Kilimo - Tizeba - Mwanjelwa
Mifugo/uvuvi - Mpina - Urega
Nje - mahiga - Kolimba
Ulinzi - Mwinyi
Maji - Kamwele - Awoshio
Viwanda/biashara - Mwijage - Manyanya
Elimu - Ndalichako - Ollenasha
Afya - Ummy Mwalimu - Faustine
Tamisemi - Jafo - Serukamba na Kakunda
Mazingira - January Makamba - Lugola
Vijana - Mwamgama - Mavunde na Kipupa
Katibu bunge - Kagaigai
Source TBC 1.
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) ametangaza tarehe mpya ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais baada ya mahakama ya juu ya nchi hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.
Tangazo hilo limesema, kuwa uchaguzi huo sasa utafanyika Oktoba 26, ikiwa pia ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee atakayekuwa akitimiza miaka 56.
Wafula Chebukati awali alitangaza uchaguzi huo ufanyike Oktoba 17, mwaka huu.
Amesema, mabadiliko hayo yamekuja kwaajili ya kuwaruhusu Tume "Kuendesha uchaguzi ambao utakaokidhi viwango na masharti yaliyowekwa na mahakama ya juu ya nchi hiyo".
Jopo la majaji hivi karibuni walibatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, katika hukumu yao kufuatia kesi iliyofunguliwa na upande wa upinzani ikiongozwa na mgombea urais Raila Odinga walipoinga matokeo hayo kwa madai uchaguzi huo haukuwa wa haki na uwazi na kwamba mfumo wa kielektroniki uliingiliwa, madai ambayo Mahakama hiyo iliyounga mkono.
Utekelezaji wa agizo la rais John Magufuli la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia ujenzi wa uzio wa eneo la machimbo ya Tanzanite lililopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, limeanza kufanyiwa kazi mara moja.
Mapema leo, Meja Jenerali, Michael Isamuhyo amewasili katika eneo la vitalu A mpaka D katika eneo hilo la machimbo ya Tanzanite Mirerani na kuanza ukaguzi wa mwisho tayari kwaajili ya kuanza kazi ya kujenga uzio wa kuzunguka eneo hilo ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana nchini Tanzania pekee.
Meja Jenerali huyo aliwasili katika eneo hilo kwa helkopta maalumu iliyomteremsha katika uwanja wa wazi wa Mirerani na kupokelewa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro.
Mara baada ya kutua katika eneo hilo, Meja Jenerali Michael Isamuhyo alitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A hadi D pamoja na vichaka vilivyozunguka eneo hilo huku akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa maeneo hayo.
Pamoja na hilo, meja Jenerali Michael Isamuhyo pia alioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo hilo la madini ya Tanzanite.
Source: Azam TV
Dar es salaam. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji kwa mtoto mdogo na kumwekea valvu mbili za moyo za bandia.
Teknolojia hiyo ambayo ni nadra kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, imefanyika chini ya jopo la madaktari kutoka Taasisi ya Moyo BLK ya India na JKCI, ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Akizungumza baada ya upasuaji huo, daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, Peter Kisenge amesema kwa msaada wa wataalamu kutoka BLK wamefanikiwa kukamilisha upasuaji huo.
Amesema JKCI imekuwa ikifanya upasuaji wa kuweka valvu moja pekee, upasuaji ambao kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka jana.
"Upasuaji huu umewezekana kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kwa msaada wa BLK. Mgonjwa huyu angepelekwa nje ingegharimu zaidi ya Sh35 milioni," amesema Dk Kisenge.
Amesema upasuaji huo umegharimu Sh14 milioni.
Mwenyekiti wa BLK ambaye ni daktari bingwa wa mishipa mikubwa ya damu, Dk Ajay Kaul amesema wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha inafanikiwa katika matibabu.
Source: Habari Sasa blog
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, mahala popote duniani.
Kwa maelezo ya waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema serikali itatekeleza jambo hilo pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia ya kiongozi huyo na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu uhitaji wa matibabu zaidi ya mgonjwa.
Waziri Mwalimu amesema hayo leo Alhamisi Septemba 21, jijini Tanga, alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Azam TV, Mariam Shedafa, aliyopo mkoani Tanga, kiongozi huyo pia amesema wao kama serikali, wanashangazwa kuona watu wanachangishana mitandaoni kama vile mhimili huo wa nchi haupo.
Waziri Mwalimu amesema kwa upande wao wanaona jambo hilo limegubikwa na mambo ya kisiasa.
Source: Azam Tv
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ameitisha mazungumzo ya kitaifa yatakayomaliza vita vya vya miaka mitatu vya wenyewe kwa wenyewe.
Waasi nchini Syria wametangaza mpango wa kuondoka katika maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti mashariki mwa Aleppo.
Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii, Jamii Forums, hajafikishwa mahakamani kwa kile kinachoelezwa bado uchunguzi unaendelea.
Maonyesho ya kwanza ya biashara kwa bidhaa zinazotengenezwa Rwanda yafanyika ili kuhamasisha raia wa nchi hiyo kupenda vya kwao..
Watu kadha wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la makazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Polisi na wanajeshi kwa sasa wanafanya msako na kushika doria mjini. Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.
Eneo lililoshambuliwa huishi sana watu kutoka nje ya mji huo ambao si wa jamii ya Wasomali.
Maafisa wa polisi waripoti kwamba watu wanne wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa.
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo inaadhimisha siku tatu za maombolezi kufuatia mauaji ya raia 30 siku ya Jumamosi.
Jeshi limelaumu waasi wa ADF kwa vifo hivyo katika kijiji cha Rwangoma karibu na mji wa Beni Kaskazini mwa mkoa wa Kivu.
Raisi kabila akiwa ziarani katika eneo hili la mashariki mwa congo,ametangaza kwenye vyombo vya habari kupitia msemaji wa serekali kwamba, mauaji yanayo tendeka mjini BENI yanapashwa kuchukuliwa kama tishio la kigaidi .
Kabila alisisitiza kwamba ametowa wito mara kadhaa katika mikutano ya ICGLR,Amewataka raia wa DRC kushikamana katika siku tatu hizi za maombolezo ambapo bendera ya yaifa inapepea nusu mlingoti.Licha ya serekali
kutoa idadi ya 36 mashirika ya kiraia imetangaza hivi punde idadi ya watu 52 na kusema kuna uwezekano wa idadi hiyo kupanda.
Serikali na Umoja wa Mataifa umelilaumu kundi hilo kwa ghasia za kila mara katika eneo hilo. Makumi ya waandamanji walikongamana mjini Beni baada ya
shambulio hilo la siku ya Jumamosi. Wakibeba mmoja wa mwili wa waathiriwa hao ,waliimba nyimbo dhidi ya serikali kulingana na shahidi aliyezungumza na kituo cha habari cha AFP.
Jeshi limelaumu waasi wa ADF kwa vifo hivyo katika kijiji cha Rwangoma karibu na mji wa Beni Kaskazini mwa mkoa
wa Kivu. Serikali na Umoja wa Mataifa umelilaumu kundi hilo kwa ghasia za kila mara katika eneo hilo. Makumi ya waandamanji walikongamana mjini Beni baada ya shambulio hilo la siku ya Jumamosi. Wakibeba mmoja wa mwili wa waathiriwa hao ,waliimba nyimbo dhidi ya serikali kulingana na shahidi aliyezungumza na kituo cha habari cha AFP.
Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia Jumapili saa saba mchana nyumbani kwake katika kijiji cha Mji Mwema, eneo la kigamboni jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohamed Aboud, mwili wa Mzee
Aboud Jumbe Mwinyi ambaye pia alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa
kusafirishwa Jumatatu kwa ndege kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maziko.
Bwana Mohamed Aboud amesema Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Migombani, Mkoa wa Mjini Maghrib mnamo saa saba za mchana. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 alizaliwa June 14, 1920 huko Juba, Sudan Kusini.
Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kuhudhuria maziko hayo ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara tu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa visiwa hivyo Abeid Amani Karume. Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984.
Mungu alizale roho ya Marehemu mahali pema peponi
Ester Mbaga, mama wa Sarafina Gumbo (pichani) anatafutwa. Amepotea tangu mwaka jana Oktoba 26, 2015 juhudi za kumtafuta zinafanywa na ndugu, jamaa, marafiki na Binti yake aishie Marekani zikiwa bado hazijafanikiwa.
Mara ya mwisho Mama Sarafina(Ester Mmbaga) alionekana maeneo ya Mbezi Makonde, Mtaa wa Bunge Road, Jijini Dar e Salaam akiwa ameongozana na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Gamaeli Mwasumbi maarufu kwa jina la “Gama” mwenyeji wa Mbezi Beach.
Tangu siku hiyo ya Jumapili tarehe 26 Oktoba, 2015 alitoweka kusikojulikana huku vitu vyake vilivyokuwepo kwenye nyumba yake aliyokuwa anaishi vikiwa vimeondolewa.
Aidha, Juhudi mbalimbali za kumtafuta mama Sara Mmbaga zimefanyika bila mafanikio tangu alipopotea ambapo taarifa ya kupotea kwake ziliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kawe pamoja na vituo mbalimbali vya Habari hapa nchini.
Tunaomba watu, mtu yeyote atayeweza kumuona basi anaweza kutoa taarifa kituo cha Polisi kilichokaribu naye.
Tunajua ni jinsi gani maumivu anayoyapata Mtoto wake kipenzi wa pekee Sarafina lakini tunamuombea kwa
Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake wamrudishe Mama Sara akiwa salama salimin kwenye himaya yake.
Tunapenda kumwambia Sarafina kuwa aendelee kumwamini Mungu kwa maana kila hatua azikabidhizo kwake na kumwamini basi Mungu atamtendea muujiza.
Kuna hofu kuwa Sudan kusini huenda ikatumbukia tena kwenye vita vya kiraia.
Walioshuhudia wanasema wamesikia milio ya risasi katika mji muhimu wa Yei, kusini magharibi mwa Juba, kwenye
barabara inayounganisha Juba na taifa jirani la Uganda. Vikosi vitiifu kwa naibu rais, Riek Machar, vinasema kwamba vikosi vya serikali viliwashambulia katika maeneo yao siku ya jumamosi.
Mwezi uliopita vikosi vtiifu kwa rais Salva Kiir na Riek Machar vilikabiliana mjini Juba, katika makabiliano yaliyoifanya UN kutuma walinda 400 zaidi nchini humo.
Hata hivyo Bw Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatashirikiana tena na
umoja huo. Kila upande mara kwa mara hutupiana lawama lakuanzisha vita.
Uhasama wa kisiasa baina bwana Kiir na bwana Machar uliishia kuwa mapigano mwaka 2013. Wawili hao walitia saini mkataba wa amani mwaka 2015, japo mapigano ya mara kwa mara yamekuwa yakiendelea baina ya pande hasimu.
Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya hivi karibuni, linasema shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.
Mshirikishe mwenzako Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio na uwanjani kushinda nishani tatu za dhahabu katika michezo ya olimpiki, baada ya kuwaonyesha wakenya na waethiopia kivumbi, na kushinda mbio za mita 10,000 mjini Rio.
Mwanariadha huyo, aliye na umri wa miaka 33, alijikwaa wakati wa mbio hizo, japo alijikakamua vilivyo katika mita
100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27 sekunde 5.
Mkenya Paul Tanui ameshinda nishani ya fedha, huku mwanariadha wa Ethiopia Tamirat Tola akimaliza wa tatu. Farah atarejea uwanjani jumatano kutetea taji lake la mbio za mita 5,000, aliloshinda miaka minne iliyopita mjini
London.
"Nimeshinda dhahabu tatu kwa wanangu watatu,," Farah alisema. "Ningetaka kushinda dhahabu ya nne katika mbio
za mita 5,000 kwa mtoto wangu mchanga." Iwapo atashinda mbio hiyo, ataafikia mafanikio sawa na ya mwanariadha wa Finland Lasse Viren aliyehifadhi mataji mawili ya olimpiki katika mbio za mwendo mrefu mwaka wa
1976.
Hata hivyo Mo Farah alipata ushindani mkubwa kutoka kwa Mkenya Paul Tanui, na ilimbidi atumie nguvu za ziada kuongoza mbio hizo.
Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa lkatika juhudi za kupung...