WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumapili, 14 Agosti 2016

Mo Farah historia kwa kushinda mbio za mita 10,000

Mshirikishe mwenzako Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio na uwanjani kushinda nishani tatu za dhahabu katika michezo ya olimpiki, baada ya kuwaonyesha wakenya na waethiopia kivumbi, na kushinda mbio za mita 10,000 mjini Rio.

Mwanariadha huyo, aliye na umri wa miaka 33, alijikwaa wakati wa mbio hizo, japo alijikakamua vilivyo katika mita
100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27 sekunde 5.

Mkenya Paul Tanui ameshinda nishani ya fedha, huku mwanariadha wa Ethiopia Tamirat Tola akimaliza wa tatu. Farah atarejea uwanjani jumatano kutetea taji lake la mbio za mita 5,000, aliloshinda miaka minne iliyopita mjini
London.

"Nimeshinda dhahabu tatu kwa wanangu watatu,," Farah alisema. "Ningetaka kushinda dhahabu ya nne katika mbio
za mita 5,000 kwa mtoto wangu mchanga." Iwapo atashinda mbio hiyo, ataafikia mafanikio sawa na ya mwanariadha wa Finland Lasse Viren aliyehifadhi mataji mawili ya olimpiki katika mbio za mwendo mrefu mwaka wa
1976.

Hata hivyo Mo Farah alipata ushindani mkubwa kutoka kwa Mkenya Paul Tanui, na ilimbidi atumie nguvu za ziada kuongoza mbio hizo.