Polisi mkoani Morogoro inamshikilia diwani wa kata ya Mkwatani wilaya ya Kilosa Hussein Hassan Mwinchea kwa tuhuma yakumuua kwa kumfyatulia risasi mfugaji aliyejulikana kwa jina la Moringe Kandiri miaka 33 mkazi wa Mazoka wilayani humo baada ya kutokea vurugu baina ya wafugaji na wakulima.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro SACP Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea juni 22 majira ya saa 7 mchana huko maeneo ya Kisaki mashambani Mkwatani wilayani humo, ambapo diwani huyo aliamua kufyataua risasi hiyo baadaya ya kuvamiwa na wafugaji waliotaka kumpiga kutokana yeye kutaka kuamlia ugomvi ulioibuka kati ya kundi la wafugaji na wakulima.
Aidha kamanda wa polisi mkoani hapa mkoani hapa amesema tayari askari wameshapelekwa kwa wingi kwenye maeneo yote mawili ambayo ni tete kutokana na uhasama ulipo kati ya makundi ya wakulima na wafugaji ili kudhibiti watu wasijichukulie sheria mkononi