Benki kuu ya Tanzania (BoT) imepanga kuondoa noti zote za shilingi mia tano ndani ya miezi minne ijayo kutokana na uchakavu.
Mkurugenzi wa kurugenzi ya usimamizi wa mabenki Martian Kobelo amesema sarafu za shilingi mia tano zimeshasambazwa kuziba pengo la noti na wananchi wanapaswa kupeleka noti ili zoezi liende kwa haraka.