Wabunge wa kambi ya upinzani bungeni leo wameamua kutumia mtindo mpya wa kuziba midomo yao na kutoka njeya ukumbi wa Bunge kuendelea kupinga vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu spika.
Wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha Bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-MAGEUZI), James mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kuonyesha hisia zao na msimamo wao baada ya bunge kukataa kuwasikiliza hoja zao.