WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumanne, 21 Juni 2016

Tiketi za kielekroniki zaanza kutumika kwenye mabasi ya mwendo kasi

Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa lkatika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.

Wauzaji wa tiketi hizo MaxMalipo na Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kitengo chake cha mradi wa mabasi yaendayo haraka wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tano na mnunuzi atahitaji kusajil ili hata kama kadi yake itapotea akiba ya fedha iliyokuwa imebaki iingizwe kwenye kadi mpya atakayopewa.

Mkurugenzi mtendaji wa UdaRT, David Mgwassa amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa  katika vituo vikuu vya mabasi vya Kimara, Ubungo, Morocco, Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Afrika ambao ndiyo watengenezaji wa kadi hizo, Juma Rajab amesema bei ya kadi hiyo ni Sh 5,000 na itakuwa na Sh 4,500 ndani yake ambazo abiria anaweza kuzitumia kama nauli kwa safari nane.

Ameaema kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kuwa kiwango cha juu kitakachowekwa katika kadi hiyo ni Sh30,000.