WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatano, 15 Juni 2016

Waganga wakuu wa Mikoa watakiwa kuacha urasimu kwenye ugawaji wa Damu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kuondoa urasimu katika ugawaji damu kitendo ambacho kimekuwa kikisababisha baadhi ya wanawake wajawazito kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha takribani wanawake 432 kati ya wazazi laki moja hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tatizo la uzazi hapa nchini ambapo asilimia themanini ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa damu.