WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatano, 25 Mei 2016

Waziri wa Elimu avunja bodi ya TCU

Serikali Yaivunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU....Ni baada ya kupitisha Majina ya wanafunzi 486 wasio na Sifa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania(TCU ) kufuatia Tume hiyo kupitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.

Pia,Waziri Ndalichako amewasimamisha kazi Maafisa kadhaa waandamizi wa TCU kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema wajibu wa TCU. Waziri Ndalichako amewateua Makaimu wa nafasi za waliosimamishwa. Habari zaidi zitafuata