Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani.
Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville. Muhammad Ali alifariki Ijumaa akitibiwa Arizona wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.
Swala hiyo imerushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani.
Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu.
Maelfu ya watu wamehudhulia swala hiyo
Mazishi yake yatafanyika Ijumaa