WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 21 Septemba 2017

Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu ya Lissu


Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, mahala popote duniani.

Kwa maelezo ya waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema serikali itatekeleza jambo hilo pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia ya kiongozi huyo na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu uhitaji wa matibabu zaidi ya mgonjwa.

Waziri Mwalimu amesema hayo leo Alhamisi Septemba 21, jijini Tanga, alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Azam TV, Mariam Shedafa, aliyopo mkoani Tanga, kiongozi huyo pia amesema wao kama serikali, wanashangazwa kuona watu wanachangishana mitandaoni kama vile mhimili huo wa nchi haupo.

Waziri Mwalimu amesema kwa upande wao wanaona jambo hilo limegubikwa na mambo ya kisiasa.

Source: Azam Tv