WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumanne, 25 Oktoba 2016

Wanamgambo washambulia Mandera, Kenya

Watu kadha wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la makazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Polisi na wanajeshi kwa sasa wanafanya msako na kushika doria mjini. Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.

Eneo lililoshambuliwa huishi sana watu kutoka nje ya mji huo ambao si wa jamii ya Wasomali.

Maafisa wa polisi waripoti kwamba watu wanne wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa.

Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.