Raisi wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaachia huru wafungwa 61 walio hukumiwa kunyongwa ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wafungwa walio hukumiwa kunyongwa kupewa msamaha
Raisi Magufuli ametoa msamaha huo katika sherehe za miaka 56 ya uhuru wa Taifa hilo zilizo fanyika mjini Dodoma ikiwa ni kwa mara ya kwanza zina fanyika nje ya jiji la Dar es salaam