AU: HATUTORUHUSU KUONA MAPINDUZI YA KIJESHI ZIMBABWE.
Rais wa Guinea ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) amekariri msimamo wa muungano huo na kusema hautakubali
"mapinduzi ya kijeshi" Zimbabwe, shirika la habari la AFP limemnukuu akisema.
"Tunataka katiba iheshimiwe na mfumo wa utawala wa kikatiba urejeshwe. Hatutakubali mapinduzi ya kijeshi."
Tunafahamu kwmaba kuna matatizo ya ndani. Haya yanafaa kutatuliwa kisiasa ndani ya chama cha Zanu-PF na si kwa uingiliaji wa jeshi"
Source: bbc swahili