WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Ijumaa, 22 Septemba 2017

Marudio ya uchaguzi kenya ni October 26

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) ametangaza tarehe mpya ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais baada ya mahakama ya juu ya nchi hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

Tangazo hilo limesema, kuwa uchaguzi huo sasa utafanyika Oktoba 26, ikiwa pia ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee atakayekuwa akitimiza miaka 56.

Wafula Chebukati awali alitangaza uchaguzi huo ufanyike Oktoba 17, mwaka huu.

Amesema, mabadiliko hayo yamekuja kwaajili ya kuwaruhusu Tume "Kuendesha uchaguzi ambao utakaokidhi viwango na masharti yaliyowekwa na mahakama ya juu ya nchi hiyo".

Jopo la majaji hivi karibuni walibatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, katika hukumu yao kufuatia kesi iliyofunguliwa na upande wa upinzani ikiongozwa na mgombea urais Raila Odinga walipoinga matokeo hayo kwa madai uchaguzi huo haukuwa wa haki na uwazi na kwamba mfumo wa kielektroniki uliingiliwa, madai ambayo Mahakama hiyo iliyounga mkono.