WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 21 Septemba 2017

Jwtz kutekeleza agizo LA rais mererani

Utekelezaji wa agizo la rais John Magufuli la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia ujenzi wa uzio wa eneo la machimbo ya Tanzanite lililopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, limeanza kufanyiwa kazi mara moja.

 Mapema leo, Meja Jenerali, Michael Isamuhyo amewasili katika eneo la vitalu A mpaka D katika eneo hilo la machimbo ya Tanzanite Mirerani na kuanza ukaguzi wa mwisho tayari kwaajili ya kuanza kazi ya kujenga uzio wa kuzunguka eneo hilo ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana nchini Tanzania pekee. 

 Meja Jenerali huyo aliwasili katika eneo hilo kwa helkopta maalumu iliyomteremsha katika uwanja wa wazi wa Mirerani na kupokelewa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro.

 Mara baada ya kutua katika eneo hilo, Meja Jenerali Michael Isamuhyo alitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A hadi D pamoja na vichaka vilivyozunguka eneo hilo huku akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa maeneo hayo.

Pamoja na hilo, meja Jenerali Michael Isamuhyo pia alioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo hilo la madini ya Tanzanite.

Source: Azam TV