Mahakama kuu ya Uganda imemwachia kiongozi wa upinzani Dr. Kizza Besigye kwa dhamana. Besigye, aliyegombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita, alikamatwa tarehe 13 Mei kwa madai ya uhaini kufuatia kusambaa kwa video iliyoonyesha akiapishwa kama rais wa Uganda.