Jumla ya wanafunzi 24,528 ambao ni zaidi ya robo ya wenye sifa ya kujiunga na kidato cha tano wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato hicho na shule za ufundi kutokana na uhaba wa shule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alitoa takwimu hizo jana akibainisha kuwa hata hivyo, ufaulu kwa wanafunzi hao kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka jana.
Simbachwene alisema majaliwa ya wanafunzi waliokosa shule, ni kusubiri uchaguzi wa pili baada ya muda wa kuripoti kuwadia na kusiwe na wanafunzi waliochaguliwa lakini hawakuripoti kwenye shule za Serikali.
Kati ya waliokosa nafasi hizo, wasichana ni 6,789 na wavulana 17,739 na 348 ambao wameachwa kwa sababu umri wao umezidi miaka 24 inayotakiwa.
Wanafunzi 625 wamekosa sifa kutokana na ufaulu wao kutokuwa na masomo ya mlingano (tahasusi).
Katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, wanafunzi 393,734 walifanya mtihani na kati yao 90,380 (wasichana 36,005 na wavulana 54,375) walifaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu na hao ndiyo walioshindanishwa kujiunga na kidato cha tano,” alisema Simbachawene.
Alisema wanafunzi hao watapangwa katika shule 326 zikiwamo mpya 47 na muhula wa masomo unatarajia kuanza Julai 11 na wanatakiwa kuwa wameripoti shuleni si zaidi ya Julai 25.
Simbachawene alisema asilimia 52 ya wanafunzi waliochaguliwa ambao ni 34,064 watajiunga kwa masomo ya sayansi wakiwamo wavulana 20,598 na wasichana 13,466.
“Kwa masomo ya Sanaa na Biashara wamechaguliwa wanafunzi 30,897, kati yao wasichana ni 15,445 na wavulana 15,452.
Wanafunzi wanaokwenda vyuo vya ufundi ni 759 kati yao wasichana wakiwa 220 na wavulana