Wafanyabiashara wa gereji za kutengeneza magari na kuponda vyuma chakavu katika eneo la Sido Ungalimitedi jijini Arusha wamefunga baadhi ya mitaa na kufanyakazi zao katikati ya barabara na kuzuia shughuli zingine za kijamii kwa madai ya kukosa eneo la kufanyiakazi hali inayolalamikiwa na wakazi wa jiji la Arusha huku uongozi wa mkoa ukidai umeshatoa notisi ya kuwataka waondoke kwenye eneo hilo.