Watu 50 sasa wanajulikana kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wa shambulizi lililotokea kwenye baa moja katika jimbo la Florida, na kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi katika historia ya Marekani.
Watu wengine 50 wako hospitalini. Vyombo vya habari vimemtambua mwanamme ambaye alitekeleza shambulizi hilo katika mji wa Orlando kuwa raia wa Marekani, Omar Mateen.
Omar Mateen, aliyefyatua risasi Orlando
Mwanamme huyo wa umiri wa miaka 29, alikuwa amejihami kwa bunduki mbili wakati alifyatua risasi katika baa ya Pulse siku ya Jumaosi
Aliwashika mateka karibu watu 30 kabla ya polisi kumpiga risasi na kumuua.