Serikali imepanga kuujenga uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa kwa kiwango cha lami na kuwezesha ndege kubwa kutua katika kiwanja hicho hali itakayochochea ukuaji wa sekta ya utalii katika eneo hilo.
Kiwanja cha ndege cha nduli ni kiungo kikubwa katika kukuza sekta ya utalii mkoani Iringa na eneo la nyanda za juu kusini kutokana na uwepo wa hifadhi ya taifa ya Ruaha ambapo mkakati huu wa Serikali kujenga uwanja huu wa ndege pamoja na barabara iendayo hifadhini Ruaha vitaufanya mji wa Iringa kuwa kitovu cha utalii