Jeshi la polisi limeanzisha uchunguzi kubaini dhidi ya madai ya kupuliziwa hewa ya sumu ofisini kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa jeshi hilo tayari limewahoji watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo lililotokea Juni 13, mwaka huu.
Juhudi za kumpata Meya Bwire kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa tangu juzi na jana baada ya mtu aliyepokea simu yake ya kiganjani kujibu kuwa amepumzika na madaktari wameagiza asisumbuliwe.
Madai ya sumu kupulizwa ofisini kwa Meya huyo yaliibuka muda mfupi baada ya kiongozi huyo kuingia ofisini akitoka kwenye ziara ya kukagua maeneo yalitotengwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Sinai.