Serikali imekamata makontena mia moja na tatu (103) yaliyosheheni magogo ya Maliasili ambayo yameingia nchini kinyume cha taratibu wahusika wakiwa bado hawajafahamika.
Makontena 47 ya magogo hayo yametoka nchini Congo na mengine 56 kutoka Zambia.
Serikali ya Tanzania na Zambia zimeingia kwenye ukurasa Mpya wa kupambana na wimbi la usafirishaji na uingizaji haramu wa Magogo kinyume cha Sheria, na hivyo Mkutano mwingine wa kuendeleza juhudi hizo unatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao jijini Mbeya.