WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Ijumaa, 10 Juni 2016

Kanisa latupiwa viombo nje sinza

Kanisa la Sinza Christian Center latolewa vyombo nje Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumza na Dar es salaam yetu Blog  mke wa mmiliki  wa jingo Hilo Bi. Patricia Prosper alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu.”

Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.