Kikao cha kamati ya fedha na uongozi cha halmashauri ya Jiji la Mwanza, kimevunjika baada ya Meya Bw.James Bwire kulalamikia harufu kali, inayohisiwa kuwa ni sumu, ilikuwa ikitoka kwenye kiyoyozi ndani ya ofisi yake, huku watumishi wawili wa jiji hilo wakishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.Meya James Bwire, ambaye mwezi wa April mwaka huu alilazwa Jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kudaiwa kuanguka gafla ofisini kwake.