WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatatu, 13 Juni 2016

Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kusimamishwa kazi baada ya kudanganya kuhusu watumishi hewa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ameziagiza Mamlaka husika kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ahmed Sawa kwa tuhuma za kumdanganya juu ya suala la watumishi hewa.

Imebainika kuwa Mkurugenzi huyo alitoa taarifa zisizo za kweli akidai kuwa Mkoa huo hauna watumishi hewa tofauti na utafiti uliofanya na kamati maalum iliyoundwa na kugundua watumishi hewa 23 kutoka mkoani humo.

Kuhusu uhaba wa sukari Mkoani Iringa amesema Mkoa unaendelea na juhudi za kukabiliana na tatizo hilo na kuwatoa hofu wakazi wa Mkoa huu hususani walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa sukari itaanza kupatikana zaidi kuanzia jumatatu.