Mapigano mazito yameripotiwa kwenye eneo la mpaka kati ya Eritrea na Ethiopia Jumapili. Vikosi vya nchi zote mbili vimeshambuliana vikali ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Eritrea kusherekea uhuru wake wa miaka 25 kutoka kwa majirani zao Ethiopia
Eritrea wamelalamikia vikosi vya Ethiopia kuanza mashambulizi hayo . Mapigano hayo yameanza muda mfupi baada ya Umoja wa mataifa (UN) kutoa ripoti ikishutumu uongozi wa Eritrea chini ya utawala wa Rais Isaias Afwerki kufanya uhalifu dhidi ya binadamu.