Katika Copa America Brazil wametupwa nje ya mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0.
Bao la utata dhidi ya Peru kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi B huku timu za Peru na Ecuador zikifanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali.
Hii ni mara ya kwanza tangu 1987 kwa Brazil kushindwa kuvuka hatua ya makundi ya mashindano haya. Bao la Peru lilifungwa na Raul Ruidiaz, mfungaji akitumia mkono kufunga bao na kuleta utata mkubwa. Leo Jumanne Mexico inacheza na Venezuela huku Uruguay ikichuana na Jamaica