WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumanne, 14 Juni 2016

Tundu Lissu na Mhariri wa Mawio kizimbani Leo Kwa Uchochezi

Serikali itawafikisha Mahakama ya Kisutu leo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa kuandika habari za uchochezi.

Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.

“Nimekuja kama ilivyo amri kufika hapa kila siku asubuhi, ila nimeambiwa kesho ( leo )  tunatakiwa kufika mahakamani na wenzangu,” alisema Mkina.

Katika kesi hiyo, atakuwapo pia mhariri na mwandishi wa habari iliyosababisha kufungiwa, Jabir Idrisa pamoja na mchapishaji wa gazeti hilo.

Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo