WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumanne, 14 Juni 2016

Pikipiki 99 za waratibu elimu zatumika kubeba abiria

Pikipiki 99 zilizotolewa kwa ajili ya waratibu elimu kata mkoani Mara zimebainika kuwa zimekuwa zikitumika kubeba abiria na kujiingizia kipato badala ya kusudio la kuwawezesha waratibu hao kufuatilia mambo muhimu ya elimu.

Akikabidhi pikipiki kumi na nne kwa waratibu elimu kata, afisa mradi wa Equip Tanzania mkoa wa Mara Mary Bukombe amesema matumizi ya pikipiki 84 zilizotolewa awali yanakatisha tamaa kutokana na waratibu kutokuzijali.
Jumla ya pikipiki 99 zimekabidhiwa kwa waratibu elimu kata katika wilaya mbali mbali mkoani humo huku hitaji likiwa ni pikipiki 178 kutokana na idadi ya kata zote zilizopo mkoa wa Mara.