Jengo lililoko eneo la akiba posta jijini Dar es
salaam limeripotiwa kuwaka moto kuanzia majira
ya jioni na chanzo cha moto huo kinasemekana ni
mtungi wa gesi kulipuka na kusababisha moto.
Inasemekana hakuna madhara makubwa kutokana
na zimamoto kufika kwa wakati katika eneo la
tukio.