WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Ijumaa, 18 Machi 2016

Waziri mkuu afuta umiliki wamashamba makubwa 11 Ngara

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameagiza
kufutwa mara moja umiliki wa mashamba
makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700
katika vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera
wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mashamba hayo hayana hati na yametelekezwa.

Alitoa agizo hilo jana alipozungumza na wakazi
wa vijiji vya Kasulo na Rwakalemera katika Kata
ya Kasulo wilayani Ngara akiwa njiani kuelekea
mkoa wa Geita.

Waziri Mkuu alilazimika kufanya mkutano huo
mapema asubuhi baada ya kuitisha uongozi wa
Wilaya ya Ngara ufike kwenye mkutano huo
kujibu kero za wananchi waliosimamisha
msafara wake wakati akielekea mjini Ngara.
Uamuzi huo ulitokana na hatua ya Waziri Mkuu
kumwita kwenye mkutano huo, Ofisa Ardhi na
Maliasili wa Wilaya, Betty Munuo aeleze
chanzo cha mgogoro wa ardhi katika vijiji
hivyo.

Munuo ambaye amehamishiwa wilaya hiyo
Agosti mwaka jana, alisema aliyakuta
malalamiko hayo na amefanya uchambuzi wa
majina ya wamiliki wote wa mashamba na
ilikuwa imepangwa wapatiwe notisi wajieleze.
Katika orodha yake, Munuo alitaja wamiliki 18
wa mashamba makubwa lakini kati yao ni
wamiliki saba tu ambao mashamba yao yana
hati na matatu ndiyo yameendelezwa wakati
manne hayajaendelezwa.

Akitangaza uamuzi wake, Waziri Mkuu
aliwataja wamiliki wa mashamba yasiyo na hati
kuwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Katibu
Mkuu Utumishi katika serikali ya awamu ya
tatu, Joseph Rugumyamheto mwenye shamba
na. 527 lenye ekari 505 lililopo Rwakalemera.
Waziri Mkuu aliagiza ifanyike sensa kubaini
kama wamiliki wa mashamba hayo yote ni
Watanzania au la.

“Haya yenye hati nataka yafanyike mapitio ya
hati zao na kubainisha ni namna gani
walipatiwa hati hizo.
‘Nataka taarifa inifikie ofisini kwangu Dar es
Salaam ifikapo Machi 20, 2016,” alisema.