Katika hali ya sitofahamu wananchi wa river side kata ya kichangani manispa ya Morogoro wanaoishi kandokando ya mto wameshuhudia maiti ya kitoto kichanga kilichotupwa na mtu asiye fahamika
Walioshuhudia tukio hilo waliona mwili wakitoto hicho ukielea ndani ya maji
" sisi tuliona kitu kikielea kwenye maji ndipo tulipo gundua kuwa nikitoto alafu kilikuwa kama bado kizima hivi ndipo tulipo amua kukitoa kwenye maji"
Wananchi hao walio utoa mwili huo kwenye maji wameomba vyombo vya usalama kuchukua hatua ya kupita nyumba kwa nyumba ili kubaini alie fanya unyama huo
Mwandishi wetu wa kinTv alie kuwa eneo la tukio alishuhudia kichanga hicho kikiibuliwa kwenye maji na raia kikiwa kimefariki dunia
Aidha mwili huo ulichukuliwa na polisi saa chache baada ya kuwahoji watu walio shudia mwilio na kuhifadhi kwaajili ya uchunguz