Chama cha wanasheria Zanzibar kimesikitishwa na kauli na onyo lilitolewa na naibu Mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar kamishna msaidizi Salum Msangi ya kuwaonya wanasheria wanaowatetea wahalifu ambapo wakibainika watakamatwa na kuunganishwa pamoja na wahalifu.
Kwa mujibu wa chama hicho kupitia Rais wake Omar Said Shaaban akitoa taarifa kwa waandishi wa habari amesema wamemnukuu afisa huyo kupitia moja ya chombo cha habari hapa Zanzibar akitoa tahadhari hiyo ya kuwakamaata wanasheria wanoshirikiana na wahlifu watakamatwa na kuwekwa ndani ili wakateteane wao kwa wao kauli ambayo chama hicho wanaiona kuwa ni kinyume na Sheria na katiba ya nchi huku akivitaka vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya afisa huyo.
Hata hivyo ITV ilimfuata kamishna msaidizi wa Polisi Salum Msangi kujua kwanini ametoa kauli hiyo ambayo iandiawa kwenda kinyume na sheria ambapo suala hilo lipo la baadhi ya wanasheria kushirikiana na wahalifu aliweka bayana.
Mkuu huyo wa upelelelezi Zanzibar amesema jeshi la polis halimzuii mwnasheria yoyete kufanya kazi zake za kuwatetea wananchi na kutoa onyo liko pale pale na hivi kariibuni jeshi hilo litawataja wansheria ambao wanafanya vitendo hivyo.
Kamishna msaidizi Salum Msangi pia amethibitisha kuwa polisi kuwakamata baadhi ya waliokuwa wawaklishi wa chama cha wananchi CUF kwa tuhuma za kupanga na kuchochea uharibifu wa mazao huko Pemba na inawatafuta wawkilishi wengine.