WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumamosi, 2 Julai 2016

TBS yapigwa marufuku kutoa alama ya shirika kwa mzalishaji asiye na Barcode.

Makamu wa Rais mama Samiah Suluhu Hassan amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Shirika la Viwango Tanzania TBS kutoa alama ya viwanga ya shirika hilo kwa mzalishaji ambaye hana alama ya utambulisho yaani Barcode ya hapa nchini.

Mama Samiah amesema hayo katika viwanja vya maonesho ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya kampuni ya Gsi ambayo moja kati ya majukumu yake makuu ni kuhimiza matumizi ya alama ya utambulisho yaani Barcode ya Tanzania

Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wameelezea kuridhishwa kwao na mwamko wa Wananchi kujitokeza katika maonesho na kusikiliza huduma zitolewazo  na kuvutiwa nazo.

katika maonesho hayo ya 40 ya sabasaba ya mwaka huu , Serikali imejikita katika kutoa elimu ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali lengo kuu ni kuwafanya wakitoka katika maonesho hayo wawe na ujuzi stahiki wa kufanya biashara kimataifa