Mazungumzo ya amani ya Burundi yanayoendelea mjini Arusha nchini Tanzania yako hatarini kuvunjika baada ya vyama vitano vilivyoshiriki katika uchaguzi wa mwaka jana nchini humo kuwasilisha barua kwa kiongozi wa mazungumzo hayo Rais mstaafu wa Tanzania Benjamini Mkapa kushinikiza kuondolewa kwenye mazungumzo hayo wajumbe watatu kwa madai kuwa watu hao walishiriki katika kusababisha machafuko nchini humo vinginevyo vyama hivyo vitajiondoa kwenye mazungumzo hayo.