WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatatu, 27 Juni 2016

Yanga uso kwa uso na TP Mazembe

TP Mazembe inashika nafasi ya 110 duniani na kwa Afrika inashika nafasi ya tatu kwa ubora, wakati Yanga inashika nafasi ya 1,733 duniani kwa ubora na Afrika nafasi ya 324.

Hatumwi mtoto dukani. Ndivyo unavyoweza kusema, kesho ni Yanga ya Tanzania na TP Mazembe ya DR Congo ikiwa ni mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

Mchezo wa kesho unazikutanisha timu zenye nafasi mbili tofauti hasa kwa ubora wa soka, lakini kama ilivyo, soka lolote linaweza kutokea uwanjani.

TP Mazembe inashika nafasi ya 110 duniani na kwa Afrika inashika nafasi ya tatu kwa ubora, wakati Yanga inashika nafasi ya 1,733 duniani kwa ubora na Afrika nafasi ya 324.

Mazembe waliotarajiwa kuwasili jana wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa kileleni mwa msimamo wa kundi A, licha ya kuwa ni mechi moja kwa kila mmoja imechezwa.

Yanga baada ya kupoteza mchezo wake ilibakia kwenye mji wa Antalya nchini Uturuki ilikokuwa ikijifua tayari kwa mchezo huo.

Tayari kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm amekwisha kusema kuwa wachezaji wake wameiva kila idara na wanachosubiri ni kukamilisha kile waliochotoka nacho Uturuki, licha ya kuwa wana machungu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria wiki iliyopita.

“Wachezaji wote wako sawasawa, kila kitu kimekamilika, tunasubiri kuingia uwanjani,” alisema kocha huyo, raia wa Uholanzi.

Mazembe inawatarajia wachezaji wake muhimu na zaidi katika safu ya ushambuliaji, akiwamo Adama Traore ambaye pia aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Mali na Mzambia, Given Singuluma. Hata hivyo, Singuluma inaelezwa huenda asicheze kutokana na kuumia mkono na atakaa nje ya dimba kwa wiki mbili.

Mchezaji mwingine ni Rainfold Kalaba ambaye anasifika kwa kufumania nyavu. Kalaba aliifungia Mazembe ilipoilaza Medeama 3-1 mjini Kinshasa.

Kikosi cha TP Mazembe kinachotarajiwa kesho kinaundwa na golikipa wa timu ya taifa ya Congo, Robert Kidiaba anayelindwa na mabeki raia wa Zambia, Jean Kasusula na Nathan Sinkala.

Wengine wanaotarajiwa kushuka dimba la taifa ni Thomas Ulimwengu, Solomon Asante, Salif Coulibaly, Daniel Adjei Nii, Marveille Bokadi na Christian Luyindama