Wadau wa uhifadhi kutoka Jamhuri ya watu wa CZECH kushirikiana na shirika la hiafadhi za taifa Tanapa wamefanikisha kumrudisha nchini Faru mweusi anayejulikana kwa jina la Eliska’s ikiwa ni mikakati ya kuongeza wanyama hao waliyo hatarini kutoweka kutokana na matukio ya ujangili yanayo tishia uhifadhi wa Tanzania.
Faru Eliska's aliwasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro majira ya saa mbili asubuhi.
Akizungumza wakati wa kumpokea Faru huyo jike mkurugenzi wa shirika la hifadhi za taifa Tanapa Alan Kijazi amesema mnyama huyo ni sehemu ya Faru waliyochukuliwa nchini miaka mingi iliyopita ambapo sasa wadau wa uhifadhi wameona pengo lillopo baada ya wanyama hao kutoweka kwa kasi kwa matendo ya ujangili wameamua kurudisha sehemu ya Faru ili kuimalisha uhifadhi wa Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick amesema serikali inasikitishwa na hatua ya watu wachache kufanya ujangili wa rasirimali za taifa na vitu vianvyo semekana kutengenezwa baada ya kuawa kwa Faru havilingani na thamani ya mnyama huyo ambaye ni uridhi wa dunia.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi taifa ya Mkomazi alipo pelekwa Faru huyo Bwana Marko Meoli amesema wamejipanga kuwalinda wanyama hao adhimu ili kuhakikisha kuwa hakuna jangili atakaye ingia kwenye eneo