Barcelona kulipa faini ya euro milioni 5.5
Klabu ya Barcelona imekubali kulipa faini ya euro milioni 5.5 kutokana na makosa waliyofanya katika ulipaji kodi kufuatia usajili wa Neymar kutoka Santos mwaka 2013.
Waendesha mashitaka wa Uhispania walikuwa wakiituhumu Klabu hiyo kwa kuficha thamani halisi ya manunuzi ya mchezaji huyo.
Barcelona ilitangaza kulipa ada ya euro milioni 57, huku euro milioni 17 zikienda kwa klabu yake ya Santos na zilizobakia zikienda kwa wazazi wa Neymar.
Lakini kampuni moja ya uwekezaji ya Brazil ambayo ilikuwa ikimiliki haki za asilimia 40 za Neymar ilidai hawajalipwa kiasi stahiki huku wachunguzi wakieleza kuwa gharama halisi walizolipa Barcelona ni euro milioni 83.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Uhispania sasa wamepata suluhu ya tatizo hilo kwa kuamua kulipa faini kutokana na makosa yaliyofanyika