Rais John Pombe Magufuli amezindua Daraja la Kigamboni hii leo na kukataa lisiitwe kwa jina lake, na kushauri liitwe "Daraja la Nyerere", jina la muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Wakati huo huo rais "alitumbua jipu" kwa kumsimamisha Mkurugenzi mkuu wa mkoa wa Dsm baada ya kusadikika ameisababishia Serikali hasara ya Tsh. 3 Bilioni baada ya kusaini mikataba yenye utata.
Aidha Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa taifa.