WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatano, 20 Aprili 2016

Wawili wafa kwenye ajali Kigamboni

Watu wawili wanasadikiwa kufariki dunia alfajiri ya leo baada ya gari aina ya HIACE kuserereka wakati ikiingia katika kivuko na kutumbukia Baharini.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto , Tayari mwili wa mtu mmoja mwenye jinsi ya kiume umepatikana  saa tatu asubuhi na jitihada za kusaka mwili wa abiria mwingine anasadikika kuwa ni mwanamke.

Kaka ambaye ni manusura wa ajali hiyo anasema, ndugu hao waliotumbukia kwenye gari  akiwemo dada yake ambaye bado jitihada za kumtafuta zinaendelea kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani MBEYA  kwenye msiba.