Turki al-Faisal ni mwanamfalme wa cheo cha juu nchini Saudi Arabia, amekosoa vikali madai ya rais wa Marekani Barack Obama kuwa nchi yake haijafanya jitihada kuisaidia Marekani kukabiliana na matatizo yaliyo eneo la mashariki ya kati. Kwa njia ya barua ya wazi mwanamfalme huyo alisema kuwa Saudi Arabia imekuwa kiongozi katika jitihada za kukabilia na kundi la Islamic state. Mwanamfalme huyo pia amesema kwa Saudi Arabia imetoa habari za kijasusi zilizozuia kutokea mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani.