Majambazi wawili wameuawa baada ya majibizano makali ya kutupiana risasi na jeshi la polisi Mabibo jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata silaha mbili moja ikiwa ya kivita aina ya SMG yenye risasi 7 pamoja Pistol aina ya Chainese ikiwa na risasi 6 ndani ya magazine.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema tukio hilo limetokea siku ya jumatatu maeneo ya Mabibo Repect majira ya saa 9 na nusu mchana ambapo majambazi hao walikuwa wamejipanga kufanya tukio la uporaji kwa raia aliekuwa anasafiri ndipo jeshi la polisi lilibaini tukio hilo na kufanya ufuatiliaji kwaajili ya kuwakamata katika eneo hilo kitendo ambacho kilisababisha majibizano ya risasi.