Mwanamuziki wa Marekani Christina Grimmie ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Orlando jimbo la Florida.
Mwanamuziki huyo alikuwa mmojawapo wa wanaomenyana katika kipindi cha muziki maarufu cha The Voice.
Amepigwa risasi wakati akitangamana na mashabiki wake baada ya kuwatumbuiza.
Polisi wanasema aliyetekeleza mauaji hayo amejiua