Wizara ya ulinzi nchini Urusi, inasema kuwa maafisa wa kijeshi wa nchi hiyo na wenzao wa Marekani, wamekubaliana kuboresha ushirikiano wao nchini Syria, baada ya Marekani kuilaumu Urusi kwa kushambulia kwa mabomu wapiganaji wa upinzani wanaowaunga mkono Kusini mwa Syria.
Msemaji mmoja ameeleza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa ya manufaa baada ya kisa hicho kilichotokea siku ya Alhamisi, huku akiongeza kuwa vikosi hivyo vya wapiganaji vilikuwa nje kabisa ya eneo la mapigano na kwamba Marekani ilishindwa kutoa mawasiliano yake kwa njia ya GPS