Serikali imeisimamisha kampuni ya kimataifa ya Sahara kutojihusisha na zabuni za uingizaji mafuta yeyote mbaka uchunguzi utakapokalimika baada ya kubaini imeingiza nchini maelfu ya tani ya mafuta ya Ndege yaliyochanganywa na petroli na kuiamuru kuingia gharama kusafisha matank ya mafuta na kuyaondoa mafuta hayo nchini.
Maamuzi hayo ya serikali yametolewa baada ya waziri wenye dhamana ya nishati na madini kutembelea maghara ya makampuni makubwa ya usambazaji mafuta nchini na kusikia malalamiko ya uwepo wa mafuta machafu ya Ndege yaliyongizwa nchini na kampuni hiyo na kusababisha hasara kubwa.
Malalamiko hayo yalimfanya waziri wa mwenye dhamana ya nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo kutoa maamuzi ya serikali baada ya kubaini ukweli kutoka kwa makampuni makubwa ya usambazaji ambayo yalidai hayawezi kuyasambaza mafuta hayo ya Ndege na tayari yanamikataba na mashirika mbalimbali ya Ndege.
Kutokana na maagizo hayo ya serikali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa serikali wa ununuzu wa mafuta kwa jumla-PBPA Bwana Michael Mjinja alielezea namna ya mafuta hayo yatakavyoondolewa amesema tayari muingizaji wa mafuta hayo ameingia nchini na kinachofanyika ni kuangalia namna atakavyoyaondoa mafuta hayo.