Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ameivunja bodi ya Tume ya vyuo vikuu nchini TCU na kuwasimamisha kazi watendaji wa bodi hiyo kwa kushindwa kusimamia suala la wanafunzi 489 wa chuo kikuu cha mtakatifu Joseph ambao hawakuwa na sifa ya kujiunga na elimu ya juu.
Aidha Waziri Ndalichako amewateua Profesa Eleuther Mwageni na Dokta Kokubelwa Katunzi kukaimu nafasi ya Bodi hiyo.
Waziri Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusiana na sakata la chuo kikuu cha mtakatifu Joseph kilichobainika kutokuwa nasifa ya kutoa elimu ya juu, Na hapa waziri Ndalichako anatumia mamlaka aliyonayo kuwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa bodi ya TCU.
Waziri wa Elimu amesema sakata la Chuo cha mtakatifu Joseph nimuendelezo ukaguzi unaoendelea hapa nchini nakuvitaka vyuo vikuu vyote visivyokuwa na sifa kujianda kwani sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.