WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumamosi, 7 Mei 2016

Uturuki ya koromea EU

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema serikali yake haitabadilisha sheria zake dhidi ya ugaidi kama masharti ya Muungano wa Ulaya ikiwa Uturuki inataka raia
wake kuondolewa visa ya usafiri ndani ya Ulaya.

Kwenye taarifa kwa runinga, kiongozi huyo alitoa maneno makali akisema kila mtu afuate njia yake, matamshi yaliyoonekana kuelekezwa kwa Muungano wa Ulaya.

''Tunachukua njia yetu nanyi chukeini yenu'',alisema Reccep tayyip Erdogan

Bwana Erdogan amesema kwamba Uturuki inakabiliwa na tisho la ugaidi. Waziri mkuu, Ahmet Davutoglu aliyeongoza mazungumzo ya
muafaka na Muungano wa Ulaya alitangaza kujiuzulu hapo

Alhamisi baada ya kutofautiana na Rais.
Kwenye hotuba hiyo Rais amesema atawasilisha mapendekezo ya kubadilisha mfumo wa utawala kutoka kwa Waziri Mkuu hadi Rais mwenye Mamlaka kupigiwa kura ya
maoni.