Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei kubwa.
Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.
Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.