WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 2 Juni 2016

Watumishi wanne Tabora wasimamishwa kazi kwa tuhuma za kuuza viwanja

Watumishi wanne wa idara ya ardhi manispaa ya Tabora wamesimamishwa kazi baada ya kubainika kuuza viwanja vya Manispaa kwa mtu zaidi ya mmoja na kuisababishia halmashauri kupata hati yenye mashaka.

Watumishi hao wamesimamishwa kazi wakati wa kikao cha baraza maalumu la madiwani, kilichokutana kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali zinazoonyesha udanganyifu katika ugawaji viwanja na kusababisha kuwepo kwa migogoro ya Ardhi.

Manispaa ya Tabora imekumbwa na wimbi kubwa la migogoro ya ardhi kutokana na baadhi ya watumishi wa idara hiyo kutumia madaraka yao vibaya