WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 2 Juni 2016

Wakuu wa mikoa wanaosua sua kwenye utengenezwaji wa madawati wapewa onyo

Naibu waziri Ofisi ya raisi, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo amewataka wakuu wa mikoa wote nchini wanaoendelea kusuasua katika zoezi la utengenezaji wa madawati kuongeza juhudi kwani hicho ndicho kipimo cha utendaji kazi kitakacho angaliwa na Rais Magufuli.

Naibu waziri Jaffo amesema hayo wakati wa ufunguzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Nzuguni manispaa ya Dodoma.

March 15, mwaka huu Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli wakati wa kuwaapisha wakuu wa mikoa, alisema kipimo kitakachotumika kupima utendaji kazi wakuu wa mikoa hao ni Suala la utengenezaji madawati ifikapo june 30 mwaka huu.